Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST)  Profesa Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, fursa zitolewazo na Jopo la Kimataifa la Sayansi na Mabadiliko ya Tabia nchi (IPCC) zitajulikana mapema na kuwa rahisi kuzipata  endapo watafanya kazi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).  

Prof. Kipanyula amesema hayo Machi 26,2024 alipokutana na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw. Ladislaus Chang’a ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi (IPCC) alipotembelea NM-AIST kwa lengo kutoa elimu juu ya mabadiliko ya tabia nchi na kuangalia namna kujenga mahusiano baina TMA na NM-AIST. 

 

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST)  Profesa Maulilio Kipanyula akiwa na sisitiza jinsi ya kutumia fursa zitakazopatikana katika ushirikiano baina ta NM-AIST na TMA .

Amesema kuwa, kutokana na uwezo taasisi ya  NM-AIST katika utoaji wa mafunzo na kufanya tafiti mbalimbali ,  utaiwezesha taasisi kushinda miradi  ambayo itakuwa inatangazwa ambayo itatoa fedha za kuwezesha tafiti zinazohusiana na mabadiliko ya hali hewa na tabia nchi kufanyika kwa wingi.

Naye Bw. Ladislaus Chang’a amesema kuwa TMA wameweka mkakati wa kuhamasisha ushiriki wa wanasayansi katika kuwasilisha tafiti zao IPCC na ameona NM-AIST ni miongoni wa taasisi zinazoweza kushiriki katika kutoa mchango kupitia tafiti zao, ili kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika maswala ya sayansi na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi duniani. 

    

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw. Ladislaus Chang’a, akitoa na anatoa mada za juu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Baadhi wa wadau wakifatilia kwa makini mada zinatolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

Kwa upande wa Kiongozi wa kituo cha umahiri cha Miundo Mbinu ya maji usafi wa mazingira na nishati endelevu Profesa Hans Komakech, ambaye ndio mwandaaji wa semina hii ametoa shukran kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa kutoa mada na kuonyesha fursa zinazopatikana katika Jopo la Kimataifa la Sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi. Na hivyo kutoa wito kwa wanataasisi kuhakikisha wanatumia ushirikiano uliojengwa ili kuzidi kufanya tatifi zenye tija kwa jamii na viwanda.

Naye, Bw. Erick Kiojo mwanafunzi wa Shahada ya Umahiri NM-AIST na mshiriki wa semina hiyo amesema kuwa, amenufaika sana na mada zilizotolewa  hususani kwa kuwaelekeza watafiti mada muhimu za kufanyia tafiti ambazo zina manufaa katika kutatua changamoto za jamii na viwanda na kushauri ushiriki wa sekta nyingine ili kutoa elimu zaidi kwa jamii.

NM-AIST na TMA  wamekubaliana kuwa na ushirikianao wenye tija kwa jamii na kubainisha  maeneo ambayo watajikita zaidi ikiwa ni pamoja na uandishi wa miradi ya  kufanya tafiti, mafunzo na kujengeana uwezo pamoja na kubadilishana wataalamu. Vilevile kuangalia changamoto zenye kuhitaji msukumo wa kitafiti kwa maendeleo ya nchi.