Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Omary juma Kipanga , alipata fursa ya kuona mtambo wa kupima ubora wa chujio la hewa kwenye gari na namna unavyofanya kazi pamoja na umuhimu wake kwa Tanzania na Afrika Mashariki alipotembelea Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Mtambo huo ambao unasimamiwa na WISE-Futures hivi karibuni  utaanza kufanya kazi kwa ushirikiano baina ya Taasisi ya Afrika ya  sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela kupitia  WISE-Futures na Shirika la Viwango Tanzania (TBS ) ili kupima ubora wa Air Cleaner za Magari nchini.

 

                                   

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mh. John Mongela (3 kushoto), amepata maelezo kuhusu namna ya upatikanaji wa nishati ya gesi (biogas), katika  Kituo umahiri  cha miundombinu na nishati endelevu WISE-Futures, katika ziara yake  alipotembelea Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Mh. Mongela alifurahishwa na kazi hiyo, pia alitoa rai kwa kituo kupanua wigo kwa kutoa huduma hiyo, kwa sehemu za magereza shule za msingi na sekondari ili kupunguza ukataji miti.