Bi Lucia Petro, (kulia)  mtafiti ambaye ni mnufaika wa ufadhili kutoka WISE-Futures aliyeiwakilisha NM-AIST   katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2021, ametangazwa Mshindiwa Tatu kwa jiko alilobuni linalotumia gesi asilia (biogas) kupika, Kuoka na kuchoma vyakula mbalimbali. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mh. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa Sherehe za kilele cha Mashindano hayo amempongeza Lucia na NM-AIST Kwa Ubunifu huo.

Kwa mara ya tatu sasa tangu mashindano ya MAKISATU kuanzishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kuibua na kukuza Wabunifu nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) kimekuwa kikitoa washindi.

Naibu Makamu Mkuu wa chuo Prof. Anthony Mshandete, kwa niaba ya NM-AIST alimpongeza Sana Bi Lucia Kwa uwakilishi mzuri wa NM-AIST kwa mara nyingine tena. Wakati huo huo Prof. Mshandete aliishukuru sana Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na wadau wote Kwa kuendelea kutambua mchango wa NM-AIST katika kuibua na kukuza Wabunifu Kwa Maslahi Mapana ya Taifa. Lucia amepata zawadi ya 2,000,000 za kitanzania na Cheti.