Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Tekinolojia ya Nelson Mandela Mipango, Fedha na Utawala Profesa Suzanna Agustino,atoa wito kwa waalimu wa masomo ya sayansi hasa hisabati, kuzidi kuwatia moyo watoto wa kike kusoma masomo hayo ili kupata wasomi wengi katika kada hiyo, pia amewataka watoto wa kike kuepuka vishawishi vinavyotokana na matumizi ya mitandao ya kijamii kabla ya muda.

Aliyasema hayo tarehe 22 Juni, 2023 wakati akifungua semina ya siku moja ya kuwafundisha na kuwapa motisha watoto wa kike iliyoandaliwa na kituo Cha Umahiri cha Miundombinu ya Maji, Usafi wa Mazingira na Nishati endelevu katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika.

Profesa Suzana , amekipongeza kituo cha Umahiri cha Miundombinu ya Maji, Usafi wa Mazingira na Nishati endelevu kwa kuandaa semina hiyo ambayo itawasaidia watoto kike kujiamini, kusoma kwa bidi na kufikia ndoto zao.

Naye Kiongozi wa Kituo Cha Umahiri cha Miundombinu ya Maji, Usafi wa Mazingira na Nishati Endelevu Profesa Hans Komakech amewataka wazazi kuwaruhusu watoto wa kike kwenda shule. Pia wasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii na hata kua maprofesa kwakua inawezekana.

Wahadhiri wanawake katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kutoka ndaki zilizopo wameelezea umuhimu wa masomo ya Sayansi na Ubunifu na kuwataka wanafunzi wasichana kua majasiri na kupigania wanachokiamini. Huku wakisisitiza waalimu kuwaelezea wanafunzi fursa zilizopo ikiwa watasoma kwa bidi masomo ya sayansi.

Kufeli sio kigezo cha kutofikia ndoto zako ya kupasana kujitadhimini kisha kuendelea na masoma hadi kufikia malengo yako” Alisema Dr. Janeth Marwa mmoja wa wahadhiri

Mzazi, kutoka Ngorongoro aliwaomba wazazi wote wa jamii ya masai kuendelea kuwathamini watoto wa kike na kutowaona kama bidhaa, ili kuwapa watoto wote haki ya kusoma wanachokipenda na baadaye kuwa viongozi bora.

Mwanafunzi kutoka Loliondo Lucy Lomayani amewashauri wanafunzi wenzie wa kike kutokukata tamaa na kusoma kwa bidii ili baadae waweze kuja kusoma katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Tekinolojia ya Nelson Mandela Mipango, Fedha na Utawala Profesa Suzanna Agustino.

Kiongozi wa Kituo Cha Umahiri cha Miundombinu ya Maji, Usafi wa Mazingira na Nishati Endelevu Profesa Hans Komakech.

Mwanafunzi kutoka Loliondo na Ngorongoro wakiwa katika ukumbi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Tekinolojia ya Nelson Mandela.